wimbo Huu unaitwa RAIS MAGUFULI AMETUTOKA
Niliutunga Siku ya Tarehe 17-03-2021 nilipopata Tu Taarifa ya kifo chake na Na Ilipofika Tarehe 19-03-2021 Niliwajulisha viongozi wa Parokia yangu ya Chang'ombe DAR na kisha nikawashirikisha Wanakwaya wenzangu wa Chang'ombe ( Chang'ombe Catholic singers) na Tuliurekodi katika Mfumo audio na video. Wimbo Huu niliutunga Maalum kwa Heshima ya Rais wetu Magufuli.
Nyimbo Nyingine ambazo nilizitunga
siku za Nyuma na zilizotumika Sana katika Maombolezo ya Rais wetu Ni Pamoja na
1 BWANA UNIFADHILI MIMI Chang'ombe Catholic singers Wimbo Huu umetumika Kama wimbo Maalum katika kipindi chote Cha Maombolezo na inasemekana wimbo Huu aliupenda Sana Hayati Magufuli enzi za uhai wake.
2 LAKINI HATA SASA ASEMA BWANA NIRUDIENI MIMI KWA MIOYO YENU YOTE. Wimbo Huu niliutunga mwaka 2004 na umekuwa ukitumika katika Matukio mengi ya Msiba na umefahamika Sana na watu wengi na unaimbwa katika mikoa mingi ya Tanzania na hata Nchi jirani ya Kenya, Uganda na D R Congo.Hata Bras Bend ya Jeshi wanautumia Sana katika Matukio haya na walianzia Kwenye Msiba wa Hayati Benjamini Mkapa Rais wa Awamu ya Tatu, pia wametumia Sana Kwenye Msiba wa JPM.
3 NIMEKOSA NIHURUMIE
4 NIMEUMBWA KWA AJILI YAKO
5 EE MUNGU WA HAKI YANGU UNIITIKIE NIKUITAPO.
Nyimbo Zote hizi zimetumika Sana katika Msiba huu mkubwa wa kitaifa.
Mtunzi na Mratibu Ni Mimi Aloyce Goden Kipangula. unaweza kuwasiliana nami kwa simu 0655 459 766/ 0754 459 766.
Pia unaweza kuzitazama Nyimbo Hizi Zote Youtube Kwenye channel yangu YENYE Jina ALOYCE GOLDEN KIPANGULA au Tafuta kwa Jina la Chang'ombe Catholic Singers. au Tafuta Wimbo wowote Kati ya hizo kwa kuandika Jina la Wimbo na Jina la Mtunzi Aloyce
Wimbo Mwingine wa Maombolezo niliutunga kwa AJILI ya Maombolezo ya Rais wetu wa Awamu ya Tatu Benjamini MKAPA nao Upo youtube Kea Jina PUMZIKA KWA AMANI BENJAMINI MKAPA -changombe Catholic Singers
Category
Show more
Comments - 45
Related videos for Rais Magufuli Ametutoka Chang'ombe Catholic Singers in Tanzania By Aloyce: